Yawe akamwambia Gideoni: “Watu unaokuwa nao ni wengi sana kwangu mimi kwa kuwatia Wamidiani katika mikono yao. Waisraeli wasipate kujisifu mbele yangu na kusema kwamba wamejiokoa kwa nguvu zao wenyewe.
Yonatani akamwambia yule kijana aliyemubebea silaha: “Kuja, tuende kwenye ile kambi ya hawa watu wasiotahiriwa. Labda Yawe atatusaidia, maana Yawe haokoi kwa kutegemea wingi au uchache wa watu.”