Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mukutano mpaka wakati mufalme Solomono alipojenga hekalu la Yawe kule Yerusalema. Walitumika kazi yao vizuri kufuatana na zamu ya kila kundi.
Watu wa ukoo wa Gersoni wakapewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Aseri, Nafutali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase kule Basani.