Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Hesabu 3:20 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

20 Wana wa Merari kwa kufuata jamaa zao: Mali na Musi. Hizi zilikuwa jamaa za Walawi kulingana na ukoo zao.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Hesabu 3:20
15 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Wana wa Yedutuni: Gedalia, Seri, Yesaya, Simei, Hasabia na Matitia. Wao walikuwa chini ya uongozi wa baba yao; na walitabiri kwa kutumia vinubi, na wakimushukuru na kumutukuza Yawe.


Etani wa ukoo wa Merari, alikuwa kiongozi wa kundi la tatu la waimbaji. Etani alikuwa mwana wa Kisi, Kisi wa Abudi, Abudi wa Maluku, Maluku wa Hasabia, Hasabia wa Amazia, Amazia wa Hilkia, Hilkia wa Amusi, Amusi wa Bani, Bani wa Semeri, Semeri wa Mali, Mali wa Musi, Musi wa Merari, Merari wa Lawi.


Walawi hawa wakaanza kazi: wa ukoo wa Kohati: Mahati mwana wa Amasai na Yoeli mwana wa Azaria; wa ukoo wa Merari: Kisi mwana wa Abudi na Azaria mwana wa Yehaleli; wa ukoo wa Gersoni: Yoa mwana wa Zima, na Edeni mwana wa Yoa; wa ukoo wa Elisafani: Simori na Yeneli; wa ukoo wa Hemani: Zakaria na Matania; wa ukoo wa Yedutuni: Semaya na Uzieli.


Makuhani waliandikishwa kulingana na jamaa zao, na Walawi waliotimiza miaka makumi mbili na zaidi waliandikishwa kulingana na kazi zao na zamu zao.


Sasa haya ni majina ya wana wa Lawi na wazao wao: Gersoni, Kohati na Merari. Lawi aliishi miaka mia moja makumi tatu na saba.


Wana wa Merari walikuwa: Mali na Musi. Hao ndio babu za jamaa za Walawi.


ukoo wa Lawi peke yake na ukoo wa Simei peke yake.


Wana wa Kohati kwa kufuata jamaa zao: Amuramu, Isihari, Hebroni na Uzieli.


Jamaa za Walibuni na Wasimei zilitokana na Gersoni; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wagersoni.


Jamaa za Wamali na Wamusi zilitokana na Merari;


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ