Hesabu 3:19 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200219 Wana wa Kohati kwa kufuata jamaa zao: Amuramu, Isihari, Hebroni na Uzieli. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Hizi ndizo ukoo za wale ambao walifanya kazi hizo: Kutoka ukoo wa Kohati, kulikuwa Hemani, kiongozi wa kundi la kwanza la waimbaji. Hemani alikuwa mwana wa Yoeli, Yoeli wa Samweli, Samweli wa Elekana, Elekana wa Yerohamu, Yerohamu wa Elieli, Elieli wa Toa, Toa wa Zufi, Zufi wa Elekana, Elekana wa Mahati, Mahati wa Amasai, Amasai wa Elekana, Elekana wa Yoeli, Yoeli wa Azaria, Azaria wa Sefania, Sefania wa Tahati, Tahati wa Asiri, Asiri wa Ebiasafu, Ebiasafu wa Kora, Kora wa Izihari, Izihari wa Kohati, Kohati wa Lawi, Lawi wa Israeli.
Walawi hawa wakaanza kazi: wa ukoo wa Kohati: Mahati mwana wa Amasai na Yoeli mwana wa Azaria; wa ukoo wa Merari: Kisi mwana wa Abudi na Azaria mwana wa Yehaleli; wa ukoo wa Gersoni: Yoa mwana wa Zima, na Edeni mwana wa Yoa; wa ukoo wa Elisafani: Simori na Yeneli; wa ukoo wa Hemani: Zakaria na Matania; wa ukoo wa Yedutuni: Semaya na Uzieli.