18 Na haya ndiyo majina ya wana wa Gersoni kwa kufuata jamaa zao: Libuni na Simei.
Wana wa Hemani: Bukia, Matania, Usieli, Sebueli, Yeremoti, Hanania, Hanani, Eliyata, Gidalti, Romamuti-Ezeri, Yosibekasa, Maloti, Hotiri na Mahasioti.
Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mukutano mpaka wakati mufalme Solomono alipojenga hekalu la Yawe kule Yerusalema. Walitumika kazi yao vizuri kufuatana na zamu ya kila kundi.
Sasa haya ni majina ya wana wa Lawi na wazao wao: Gersoni, Kohati na Merari. Lawi aliishi miaka mia moja makumi tatu na saba.
ukoo wa Lawi peke yake na ukoo wa Simei peke yake.
Wana wa Kohati kwa kufuata jamaa zao: Amuramu, Isihari, Hebroni na Uzieli.
Jamaa za Walibuni na Wasimei zilitokana na Gersoni; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wagersoni.
Uhesabu watu wa ukoo wa Gersoni kufuatana na jamaa na ukoo zao;