Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Hesabu 28:8 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

8 Wakati wa magaribi utamutoa yule mwana-kondoo mwingine kwa kuteketezwa kwa moto, pamoja na sadaka zile za ngano na za kinywaji. Itakuwa sadaka yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Hesabu 28:8
6 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Lakini matumbotumbo na miguu yake atavisafisha kwa maji. Kuhani ataiteketeza yote juu ya mazabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.


Atamushika mabawa na kumupasua, lakini asimwachanishe vipande viwili. Kisha, kuhani atamuteketeza kwenye mazabahu, juu ya kuni. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.


Lakini matumbotumbo na miguu ya nyama yule vitasafishwa kwa maji. Kuhani atateketeza sadaka yote juu ya mazabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.


Sadaka ya kinywaji itakayotolewa na kila mwana-kondoo ni litre moja ya divai. Utaimimina sadaka hii ya kinywaji kikali Pahali Patakatifu.


Siku ya Sabato, mutatoa sadaka ya wana-kondoo dume wawili wa mwaka mumoja wasiokuwa na kilema, sadaka ya vyakula ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta, na sadaka yake ya kinywaji.


Mutatoa vilevile beberu mumoja kuwa sadaka kwa ajili ya zambi, zaidi ya sadaka ya kuteketezwa ya kawaida pamoja na sadaka yake ya vyakula na sadaka yake ya kinywaji.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ