Hesabu 28:2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20022 Uwaamuru Waisraeli maneno haya: Ninyi mutanitolea kwa wakati wake sadaka zinazotakiwa: vyakula vya kuteketezwa kwa moto, vyenye harufu nzuri ya kupendeza. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Kuhani Yoyada akaweka walinzi kwa kulinda nyumba ya Yawe. Hao walinzi wakasimamiwa na makuhani na Walawi ambao Daudi aliwaweka katika kazi ya kutunza nyumba ya Yawe kutoa sadaka za kutetezwa kwa moto kwa Yawe kama vile ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, wakishangilia na kuimba kwa kufuata amri ya Daudi. Vilevile wakasimamia mambo ya uimbaji na sherehe.
kwa ajili ya mikate mitakatifu, sadaka za unga za kawaida, sadaka za kuteketezwa kwa moto za kawaida, sadaka za siku za Sabato, sikukuu za mwandamo wa mwezi, sikukuu nyingine zilizowekwa, vitu vingine vitakatifu, sadaka za kusamehewa zambi, kwa kuwafanyia upatanisho watu wa Israeli na kazi nyingine zozote za nyumba ya Mungu wetu.
Itakuwa ni mapaswa ya mufalme kuhakikisha kuwa sadaka za kuteketezwa, sadaka za vyakula na sadaka za kinywaji zinazotolewa wakati wa sikukuu ya mwandamo wa mwezi, Sabato, na sikukuu zozote zilizowekwa kwa Waisraeli, zinapatikana. Mufalme yeye mwenyewe atatayarisha sadaka za kusamehewa zambi, sadaka za vyakula, sadaka za kuteketezwa kwa moto, na sadaka za amani kwa kuwafanyia watu wote wa Israeli upatanisho.
basi, ikiwa kosa hilo limefanyika bila kukusudia, bila Waisraeli wote pamoja kujua, watatoa mwana-ngombe dume mumoja kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumupendeza Yawe, pamoja na sadaka yake ya vyakula na ya kinywaji kufuatana na maagizo yake. Vilevile watu watatoa beberu mumoja kuwa sadaka kwa ajili ya zambi.