Hawa ndio wazao wa Efuraimu: Sutela alizaa Beredi, Beredi alizaa Tahati, Tahati alizaa Eleada, Eleada alizaa Tohati, Tohati alizaa Zabadi, Zabadi alizaa Sutela. Zaidi ya hao, Efuraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa inchi ya Gati kwa sababu walikwenda kule kuwanyanganya ngombe zao.