Wengine waliobaki wa kabila la Manase walipewa sehemu yao kwa kura kulingana na ukoo zao. Ukoo hizo zilikuwa zile za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Sekemu, Heferi na Semida ambao wote walikuwa wazao wa kiume wa Manase mwana wa Yosefu.
Malaika wa Yawe akaenda, akaikaa chini ya muti wa mwalo wa Yoasi Mwabiezeri, kule Ofura. Gideoni mwana wa Yoasi alikuwa anapepeta ngano ndani ya kikamulio cha kukamulia zabibu kusudi Wamidiani wasimwone.
Lakini Gideoni akawajibu: “Mambo niliyofanya mimi si kitu kabisa yakilinganishwa na yale muliyoyafanya ninyi. Walichookota watu wa Efuraimu wakati wa mavuno ni kizuri kuliko mavuno ya jamaa yangu ya Abiezeri.