Kwa sababu watu wa Israeli, walipokuwa wanasafiri toka Misri, wao hawakuwapa chakula wala maji ya kunywa, pahali pake wakamulipa Balamu kwa kuwalaani watu wa Israeli, lakini Mungu wetu akageuza laana yao kuwa baraka.
Hii ndiyo hesabu ya vifaa vilivyotumika katika kujenga hema la kuchunga vile vibao vya agano. Hesabu hii ilitayarishwa na Walawi kwa amri ya Musa, chini ya uongozi wa Itamari mwana wa kuhani Haruni.
Yawe awatenge mbali watu wanaofanya mambo hayo kutoka kati ya wazao wa Yakobo. Na wasishiriki hata kidogo katika kutoa ushuhuda na kuleta sadaka mbele ya Yawe wa majeshi.
Hivi ndivyo, Waisraeli walivyofanya kila kitu kama vile Yawe alivyomwamuru Musa. Wakapiga kambi zao, kufuata bendera zao na wakasafiri kila mumoja akiandamana na jamaa yake kwa kufuata ukoo wake.