Jamii za watu zikutumikie, na mataifa yainame mbele yako kwa heshima. Ukuwe mutawala wa wandugu zako, na wana wa mama yako wainame mbele yako kwa heshima. Kila mutu anayekulaani alaaniwe, kila mutu anayekubariki abarikiwe!”
Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo “Ushuhuda wa mayungiyungi.” Mashairi ya Daudi ya kufundisha yanayoelekea wakati alipopigana na Wasuria katika Mesopotamia na Zoba naye Yoabu aliporudi nyuma na kuwaua Waedomu elfu kumi na mbili katika bonde la Chumvi.
Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, anayefika kutoka Bosira na nguo ya madoa mekundu? Ni nani huyo aliyevaa nguo ya utukufu, anatembea kwa nguvu zake kubwa? Ni mimi Yawe ninayetangaza ushindi wangu; nami ni mwenye nguvu ya kuokoa.
Siku inakuja nitakapoisimika nyumba ya Daudi iliyoanguka; nitazitengeneza kuta zake, na kusimika upya mabomoko yake. Nitaijenga upya kama ilivyokuwa tangu zamani.