Nimeyaweka maneno yangu katika kinywa chako; nimekuficha katika kivuli cha mukono wangu. Mimi nilizitandaza mbingu, nikaiweka misingi ya dunia. Mimi ninawaambia, enyi watu wa Sayuni: Ninyi ni watu wangu.
Yawe anasema: Mimi ninafanya nanyi agano hili: Roho wangu anayekuwa juu yenu, maneno niliyoyaweka katika kinywa chenu, hayataondoka kwenu hata kidogo, wala kwa watoto na wajukuu wenu, tangu sasa na hata milele.
Lakini malaika wa Yawe akamwambia Balamu: Kwenda na watu hawa, lakini utasema tu kile nitakachokuambia. Basi, Balamu akaendelea na safari pamoja na viongozi wa Balaki.
(Yeye hakusema maneno haya kutokana na mawazo yake mwenyewe; lakini kwa maana yeye ndiye aliyekuwa Kuhani Mukubwa mwaka ule, alitabiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa la Wayuda.