Kila siku, katika muda huo wa siku saba, atamutolea Yawe sadaka ya ngombe dume saba na kondoo dume saba wasiokuwa na kilema kwa kuwateketeza kwa moto. Tena ni lazima atoe sadaka kila siku kuwa sadaka ya kusamehewa zambi.
Basi, Balaki akamutwaa Balamu kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha mulima Pisiga. Hapo akajenga mazabahu saba na kutoa juu ya kila mazabahu ngombe dume mumoja na kondoo dume mumoja.
Halafu Balamu akamwambia Balaki: Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa kwa moto, nami niende. Labda Yawe atakutana nami. Chochote atakachonionyesha nitakuja kukuambia. Basi, Balamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mulima.