Lakini malaika wa Yawe akamwambia Balamu: Kwenda na watu hawa, lakini utasema tu kile nitakachokuambia. Basi, Balamu akaendelea na safari pamoja na viongozi wa Balaki.
Basi, Balamu akarudi, akamukuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na wakubwa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza: Yawe amekuambia nini?
Sasa Balamu akatambua kwamba Yawe alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakukwenda sawa vile mara ingine kwa kutafuta uchawi. Akaelekea kwenye jangwa,