Kisha, Balaki akamwambia Balamu: Tuende pahali pengine ambapo utaweza kuwaona; hata hivyo utaona tu sehemu yao, hautaweza kuwaona wote. Kisha uwalaani kutoka huko kwa ajili yangu.
Halafu Balamu akamwambia Balaki: Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa kwa moto, nami niende. Labda Yawe atakutana nami. Chochote atakachonionyesha nitakuja kukuambia. Basi, Balamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mulima.
Niliwaambia kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa feza na zahabu, mimi sitaweza kubadilisha agizo la Yawe, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa mapenzi yangu mwenyewe. Nilisema kwamba atakachosema Yawe ndicho nitakachosema.
Kwa maana watu wa namna hii hawamutumikii Bwana wetu Kristo, lakini wanatumikia tu tumbo yao wenyewe. Tena kwa maneno yao matamu na ya kujipendekeza wanadanganya watu wasiokuwa na makosa.