Wazao wako nitawafanya wakuwe wengi wasihesabike, kama vile mavumbi ya inchi. Kama vile vumbi isivyoweza kuhesabika, ndivyo wazao wako hawataweza kuhesabika!
Wazao wako watakuwa wengi kama mavumbi ya dunia, na urizi wao utaenea kila pahali: upande wa magaribi, mashariki, kaskazini na kusini. Kwa njia yako na ya wazao wako, jamaa zote katika dunia zitabarikiwa.
Jumla ya wanaume watakaokuwa katika kambi ya Rubeni kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja makumi tano na moja mia ine na makumi tano. Hawa ndio watakaokuwa katika kundi la pili.
Jumla ya watu waliokuwa katika kambi ya Efuraimu kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja na nane na mia moja. Hawa ndio watakaokuwa katika kundi la tatu.
Jumla ya watu waliokuwa katika kambi ya Dani kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia makumi tano na saba na mia sita. Hawa ndio watakaokuwa katika kundi la mwisho nyuma ya bendera zao.
Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja makumi nane na sita na mia ine. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.
Kwa maana, tunajua kwamba hema hii tunayoishi ndani yake hapa katika dunia, maana yake mwili wetu, itakapobomolewa, Mungu atatupatia makao mengine mbinguni. Nayo ni nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe na inayodumu milele.
Tena nikasikia sauti kutoka mbinguni, ikisema: “Andika maneno haya: ‘Heri tangu sasa kwa watu wanaokufa wakimwamini Bwana!’ ” Naye Roho anasema: “Ndiyo, ni kweli. Watapumzika toka katika masumbuko yao, kwa maana matendo yao yatafuatana nao.”