Basi, wanakuja kwako makundi kwa makundi na kuikaa mbele yako kama watu wangu, kusudi wasikie unachosema, lakini hawafanyi unachowaambia wafanye. Wanasema kwamba wana upendo, lakini hayo ni kusema tu; wanachotafuta kwa moyo ni faida yao tu.
Lakini Balamu akawajibu watumishi wa Balaki: Hata kama Balaki atanipa nyumba yake imejaa feza na zahabu, mimi sitaweza kuvunja amri ya Yawe, Mungu wangu, juu ya jambo lolote, dogo au kubwa.
Halafu Balamu akamwambia Balaki: Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa kwa moto, nami niende. Labda Yawe atakutana nami. Chochote atakachonionyesha nitakuja kukuambia. Basi, Balamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mulima.
Niliwaambia kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa feza na zahabu, mimi sitaweza kubadilisha agizo la Yawe, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa mapenzi yangu mwenyewe. Nilisema kwamba atakachosema Yawe ndicho nitakachosema.