39 Basi, Balamu akaenda pamoja na Balaki. Wakafika katika muji Kiriati-husoti.
Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao, wanapojichokesha huko juu pahali pa ibada, wanapokwenda pahali pao patakatifu kwa kuomba, hawatakubaliwa.
Balamu akamujibu Balaki: Sasa nimekuja! Lakini, nina mamlaka ya kusema neno lolote? Jambo Mungu atakaloniambia ndilo ninalopaswa kusema.
Huko Balaki akatoa sadaka ya ngombe na kondoo, akawagawanyia Balamu na wakubwa waliokuwa pamoja naye nyama.