Hesabu 22:30 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
30 Punda akamwambia Balamu: Mimi si yuleyule punda wako aliyekubeba maisha yako yote mpaka siku hii ya leo? Nimekwisha kukutendea namna hii? Balamu akajibu: Hapana.
Hapo, Yawe akafungua macho ya Balamu, naye akamwona malaika wa Yawe amesimama katika njia, akishika upanga uliochomolewa toka kifuko chake. Balamu akajitupa uso mpaka chini.