25 Punda alipomwona malaika huyo wa Yawe, akajibanisha kwenye ukuta na kubana muguu wa Balamu hapo. Kwa hiyo Balamu akamupiga tena huyo punda.
Endelea basi na uganga wako, tegemea wingi wa uchawi wako. Wewe uliyashugulikia tangu ujana wako ukitumainia kwamba utafanikiwa au kusababisha woga kwa watu!
Kisha malaika huyo wa Yawe akatangulia mbele, akasimama pahali hiyo njia ilikuwa nyembamba, kati ya mashamba ya mizabibu na kuta pande zote mbili.
Kisha malaika akatangulia tena, akasimama pahali pembamba pasipo na nafasi ya kupita kuume wala kushoto.