24 Kisha malaika huyo wa Yawe akatangulia mbele, akasimama pahali hiyo njia ilikuwa nyembamba, kati ya mashamba ya mizabibu na kuta pande zote mbili.
Basi, punda akamwona malaika huyo wa Yawe amesimama katika njia, akishika upanga uliochomolewa. Kwa hiyo akaacha njia, akaenda pembeni. Balamu akamupiga huyo punda, akamurudisha katika njia.
Punda alipomwona malaika huyo wa Yawe, akajibanisha kwenye ukuta na kubana muguu wa Balamu hapo. Kwa hiyo Balamu akamupiga tena huyo punda.