Basi, kesho yake, Abrahamu akaamuka asubui mapema, akatandika punda wake, akawatwaa watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwana wake. Akatayarisha kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto, kisha akaanza safari kuelekea pahali alipoambiwa na Mungu.