Kwa vile umefanya mipango juu yangu na nimesikia majivuno yako, nitatia ndoana yangu ndani ya pua yako, na lijamu yangu ndani ya kinywa chako. Nitakurudisha katika njia ileile uliyokuja ndani yake.
Lakini malaika wa Yawe akamwambia Balamu: Kwenda na watu hawa, lakini utasema tu kile nitakachokuambia. Basi, Balamu akaendelea na safari pamoja na viongozi wa Balaki.
Niliwaambia kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa feza na zahabu, mimi sitaweza kubadilisha agizo la Yawe, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa mapenzi yangu mwenyewe. Nilisema kwamba atakachosema Yawe ndicho nitakachosema.