Hesabu 2:3 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20023 Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki watakuwa kikundi cha watu wanaokuwa chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nasoni mwana wa Aminadabu. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Haya ni majina ya watu watakaokusaidia: Kabila la Rubeni: Elisuri mwana wa Sedeuri; Kabila la Simeoni: Selumieli mwana wa Suri-Sadai; Kabila la Yuda: Nasoni mwana wa Aminadabu; Kabila la Isakari: Netaneli mwana wa Suari; Kabila la Zebuluni: Eliabu mwana wa Heloni; Kabila la Efuraimu: Elisama mwana wa Amihudi; Kabila la Manase: Gamalieli mwana wa Pedasuri; Kabila la Benjamina: Abidani mwana wa Gideoni; Kabila la Dani: Ahiezeri mwana wa Amishadai; Kabila la Aseri: Pagieli mwana wa Okrani; Kabila la Gadi: Eliasafu mwana wa Deueli; Kabila la Nafutali: Ahira mwana wa Enani.
Musa na Haruni na wana wao watapiga kambi yao mbele ya hema takatifu upande wa mashariki, ni kusema mbele ya hema la mukutano kuelekea upande linakotokea jua. Kazi yao itakuwa kutumika kwenye Pahali Patakatifu kwa jambo lolote lililohitajika kufanyika kwa ajili ya Waisraeli. Mutu mwingine yeyote aliyesogea karibu alipaswa kuuawa.
Wale waliotoa sadaka ni hawa: Siku ya kwanza: Nasoni mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda; Siku ya pili: Netaneli mwana wa Suari, wa kabila la Isakari; Siku ya tatu: Eliabu mwana wa Heloni, wa kabila la Zebuluni; Siku ya ine: Elisuri mwana wa Sedeuri, wa kabila la Rubeni: Siku ya tano: Selumieli mwana wa Suri-Shadai, wa kabila la Simeoni; Siku ya sita: Eliasafu mwana wa Deueli, wa kabila la Gadi; Siku ya saba: Elisama mwana wa Amihudi, wa kabila la Efuraimu; Siku ya nane: Gamalieli mwana wa Pedasuri, wa kabila la Manase; Siku ya tisa: Abidani mwana wa Gideoni, wa kabila la Benjamina; Siku ya kumi: Ahiezeri mwana wa Amishadai, wa kabila la Dani; Siku ya kumi na moja: Pagieli mwana wa Okrani, wa kabila la Aseri; Siku ya kumi na mbili: Ahira mwana wa Enani, wa kabila la Nafutali. Hii ni sadaka iliyotolewa na kila mumoja: sahani moja ya feza yenye uzito wa kilo moja na nusu na beseni moja la feza lenye uzito wa grama mia nane kulingana na vipimo vya hema takatifu; sahani na beseni hilo vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya vyakula; kisahani kimoja cha zahabu chenye uzito wa grama mia moja na kumi kikiwa kimejazwa ubani; mwana-ngombe dume mumoja, kondoo dume mumoja, na mwana-kondoo dume mumoja wa mwaka mumoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; beberu mumoja kwa ajili ya sadaka ya zambi; ngombe dume wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mumoja kwa ajili ya sadaka za amani.