Hesabu 2:25 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
25 Kwa upande wa kaskazini, watapiga kambi katika jeshi lake wale wanaokuwa chini ya bendera ya Dani, kiongozi wao atakuwa Ahiezeri, mwana wa Amishadai,
Mwisho, wale waliokuwa chini ya bendera ya jeshi lililoongozwa na kabila la Dani, waliokuwa kama walinzi nyuma ya majeshi yote, wakasafiri, kundi moja nyuma ya lingine. Hawa waliongozwa na Ahiezeri mwana wa Amishadai.