Hesabu 2:24 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
24 Jumla ya watu waliokuwa katika kambi ya Efuraimu kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja na nane na mia moja. Hawa ndio watakaokuwa katika kundi la tatu.
Nyuma ya hao, wakafuata watu waliokuwa chini ya bendera ya jeshi lililoongozwa na kabila la Efuraimu, kundi moja nyuma ya lingine. Kiongozi wao alikuwa Elisama mwana wa Amihudi.
Jumla ya wanaume watakaokuwa katika kambi ya Rubeni kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja makumi tano na moja mia ine na makumi tano. Hawa ndio watakaokuwa katika kundi la pili.
Jumla ya watu waliokuwa katika kambi ya Dani kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia makumi tano na saba na mia sita. Hawa ndio watakaokuwa katika kundi la mwisho nyuma ya bendera zao.
Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na jeshi lake ni watu elfu mia moja makumi nane na sita na mia ine. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.