Hesabu 2:18 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
18 Kwa upande wa magaribi, wale wanaokuwa chini ya bendera ya kundi la Efuraimu watapiga kambi kulingana na jeshi lake kiongozi wao akiwa Elisama mwana wa Amihudi,
Yakobo akaendelea kusema: “Wana wako wawili uliowapata hapa Misri mbele sijafika, ni wana wangu. Efuraimu na Manase watakuwa wangu kama vile Rubeni na Simeoni wanavyokuwa.
Watarudi wakiwa wanatoa machozi, nami nitawaongoza nikiwafariji; nitawapitisha kando ya vijito vya maji, katika njia iliyonyooka ambamo hawatajikwaa; maana mimi nimekuwa baba wa Israeli, Efuraimu ni muzaliwa wangu wa kwanza.
Nyuma ya hao, wakafuata watu waliokuwa chini ya bendera ya jeshi lililoongozwa na kabila la Efuraimu, kundi moja nyuma ya lingine. Kiongozi wao alikuwa Elisama mwana wa Amihudi.
Utukufu wake ni utukufu wa ngombe dume wa kwanza, pembe zake ni za mbogo dume. Atazitumia kusukuma mataifa; yote atayasukuma mpaka miisho ya dunia. Efuraimu atakuwa na pembe hizo elfu kumi na Manase kwa maelfu.”