Mutatoa vitu hivi zaidi ya ile sadaka ya kuteketezwa ya mwezi mupya na sadaka yake ya vyakula, na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya vyakula na sadaka zake za kinywaji kama vile inavyoagizwa. Itakuwa harufu nzuri yenye kupendeza; ni sadaka kwa Yawe iliyoteketezwa kwa moto.