Hesabu 13:3 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20023 Basi, kwa agizo la Yawe, Musa akatuma watu kutoka jangwa la Parani. Watu wote waliotumwa walikuwa viongozi wa makabila mbalimbali ya watu wa Israeli. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Haya ndiyo majina ya watu hao kulingana na makabila yao: Kabila la Rubeni: Samua mwana wa Zakuri. Kabila la Simeoni: Safati mwana wa Hori. Kabila la Yuda: Kalebu mwana wa Yefune. Kabila la Isakari: Igali mwana wa Yosefu. Kabila la Efuraimu: Hosea mwana wa Nuni. Kabila la Benjamina: Palti mwana wa Rafu. Kabila la Zebuluni: Gadieli mwana wa Sodi. Kabila la Yosefu (ni kusema kabila la Manase): Gadi mwana wa Susi. Kabila la Dani: Amieli mwana wa Gemali. Kabila la Aseri: Seturi mwana wa Mikaeli. Kabila la Nafutali: Nabi mwana wa Wofusi. Kabila la Gadi: Geueli mwana wa Maki.