Hesabu 10:6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
6 Alama hiyo ikipigwa mara ya pili, wale wa kambi za upande wa kusini wataanza kuondoka. Alama hiyo ya baragumu itatolewa kila wakati wa kuanza safari.
Halafu, watu waliokuwa chini ya bendera ya jeshi lililoongozwa na kabila la Rubeni, wakafuata kundi moja nyuma ya lingine. Kiongozi wao alikuwa Elisuri mwana wa Sedeuri.