Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Hesabu 1:5 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

5-15 Haya ni majina ya watu watakaokusaidia: Kabila la Rubeni: Elisuri mwana wa Sedeuri; Kabila la Simeoni: Selumieli mwana wa Suri-Sadai; Kabila la Yuda: Nasoni mwana wa Aminadabu; Kabila la Isakari: Netaneli mwana wa Suari; Kabila la Zebuluni: Eliabu mwana wa Heloni; Kabila la Efuraimu: Elisama mwana wa Amihudi; Kabila la Manase: Gamalieli mwana wa Pedasuri; Kabila la Benjamina: Abidani mwana wa Gideoni; Kabila la Dani: Ahiezeri mwana wa Amishadai; Kabila la Aseri: Pagieli mwana wa Okrani; Kabila la Gadi: Eliasafu mwana wa Deueli; Kabila la Nafutali: Ahira mwana wa Enani.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Hesabu 1:5
17 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Haya ndiyo majina ya wakubwa wa kabila za Waisraeli: Kabila la Rubeni: Eliezeri mwana wa Sikiri. Kabila la Simeoni: Sefatia mwana wa Maka. Kabila la Lawi: Hasabia mwana wa Kemueli. Kabila la Haruni: Zadoki. Kabila la Yuda: Elihu, mumoja wa wandugu za mufalme Daudi. Kabila la Isakari: Omuri mwana wa Mikaeli. Kabila la Zebuluni: Isimaya mwana wa Obadia. Kabila la Nafutali: Yeremoti mwana wa Azrieli. Kabila la Efuraimu: Hosea mwana wa Azazia. Nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya. Nusu ya kabila la Manase katika Gileadi: Ido mwana wa Zekaria. Kabila la Benjamina: Yasieli mwana wa Abeneri. Kabila la Dani: Azareli mwana wa Yerohamu.


Wale waliokuwa chini ya bendera ya jeshi la kabila la Yuda, wakatangulia, kundi moja kisha lingine. Kiongozi wao alikuwa Nasoni mwana wa Aminadabu.


Halafu, watu waliokuwa chini ya bendera ya jeshi lililoongozwa na kabila la Rubeni, wakafuata kundi moja nyuma ya lingine. Kiongozi wao alikuwa Elisuri mwana wa Sedeuri.


Kwa upande wa kusini, wale wanaokuwa chini ya bendera ya kundi la Rubeni kulingana na jeshi lake, kiongozi wao akiwa Elisuri mwana wa Sedeuri,


Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki watakuwa kikundi cha watu wanaokuwa chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nasoni mwana wa Aminadabu.


Wale waliotoa sadaka ni hawa: Siku ya kwanza: Nasoni mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda; Siku ya pili: Netaneli mwana wa Suari, wa kabila la Isakari; Siku ya tatu: Eliabu mwana wa Heloni, wa kabila la Zebuluni; Siku ya ine: Elisuri mwana wa Sedeuri, wa kabila la Rubeni: Siku ya tano: Selumieli mwana wa Suri-Shadai, wa kabila la Simeoni; Siku ya sita: Eliasafu mwana wa Deueli, wa kabila la Gadi; Siku ya saba: Elisama mwana wa Amihudi, wa kabila la Efuraimu; Siku ya nane: Gamalieli mwana wa Pedasuri, wa kabila la Manase; Siku ya tisa: Abidani mwana wa Gideoni, wa kabila la Benjamina; Siku ya kumi: Ahiezeri mwana wa Amishadai, wa kabila la Dani; Siku ya kumi na moja: Pagieli mwana wa Okrani, wa kabila la Aseri; Siku ya kumi na mbili: Ahira mwana wa Enani, wa kabila la Nafutali. Hii ni sadaka iliyotolewa na kila mumoja: sahani moja ya feza yenye uzito wa kilo moja na nusu na beseni moja la feza lenye uzito wa grama mia nane kulingana na vipimo vya hema takatifu; sahani na beseni hilo vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya vyakula; kisahani kimoja cha zahabu chenye uzito wa grama mia moja na kumi kikiwa kimejazwa ubani; mwana-ngombe dume mumoja, kondoo dume mumoja, na mwana-kondoo dume mumoja wa mwaka mumoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; beberu mumoja kwa ajili ya sadaka ya zambi; ngombe dume wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mumoja kwa ajili ya sadaka za amani.


Viongozi wa Israeli na wakubwa wa ukoo na viongozi wa makabila ambao walisimamia watu wale waliohesabiwa,


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ