Makuhani wao wanavunja sheria zangu, na kukufuru vyombo vyangu vitakatifu. Hawapambanui kati ya vitu vitakatifu na vitu visivyokuwa vitakatifu, wala hawafundishi watu tofauti kati ya mambo yanayokuwa machafu na yanayokuwa safi. Wameacha kuzishika Sabato zangu, na kunizaraulisha kati yao.
Ni kazi ya makuhani kuwafundisha watu maarifa ya kweli juu ya Mungu kusudi watu wawaendee kwa kujifunza mapenzi yangu kwao, maana makuhani ni wajumbe wa Yawe wa majeshi.
Na watafundisha wazao wa Yakobo maagizo yako; watafundisha watu wa Israeli sheria yako. Walawi watafukiza ubani mbele yako, sadaka nzima za kuteketezwa juu ya mazabahu yako.
Anapaswa kushika Neno la kweli linalolingana na mafundisho yetu. Hivi ataweza kuwaonya watu kwa njia ya mafundisho ya kweli na kuwashinda wale wanaomupinga.