Ezra 3:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20029 Yesua, wana wake na jamaa yake, pamoja na Kadimieli na wana wake, (wa ukoo wa Yuda) walishirikiana kwa kusimamia ujenzi wa nyumba ya Mungu. Wakasaidiwa na wazao wa Henadadi na wandugu zao Walawi. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Basi, watu wakaanza kazi katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili nyuma ya kufikia kwenye nyumba ya Mungu katika Yerusalema. Zerubabeli, mwana wa Saltieli, Yesua mwana wa Yosadaki, wandugu zao wengine, makuhani, Walawi na watu wengine wote waliorudi Yerusalema kutoka katika uhamisho, wakajiunga nao katika kazi hiyo. Walawi wote waliokuwa na umri wa miaka makumi mbili au zaidi, walichaguliwa kwa kusimamia kazi ya kuijenga upya nyumba ya Yawe.