Hivyo wakachagua watu hawa katika ukoo za waimbaji: Hemani mwana wa Yoeli, ndugu yake Asafu aliyekuwa mwana wa Berekia na wana wa Merari, ndugu zao, na Etani mwana wa Kusaya.
Wajengaji walipoanza kuweka musingi wa hekalu la Yawe, makuhani wakiwa wamevaa nguo zao, walisimama pahali pao na baragumu katika mikono, nao Walawi wa ukoo wa Asafu wakisimama na matoazi yao, basi, wakamutukuza Yawe kufuatana na maagizo ya mufalme Daudi wa Israeli.
na Matania mwana wa Mika mwana wa Zabudi, wa uzao wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba maombi ya shukrani. Bakubukia alikuwa musaidizi wake. Pamoja nao kulikuwa Abuda mwana wa Samua mwana wa Galali wa uzao wa Yedutuni.