Yesua, wana wake na jamaa yake, pamoja na Kadimieli na wana wake, (wa ukoo wa Yuda) walishirikiana kwa kusimamia ujenzi wa nyumba ya Mungu. Wakasaidiwa na wazao wa Henadadi na wandugu zao Walawi.
Katika siku ya ine, tukiwa ndani ya nyumba ya Mungu wetu, tukapima ile feza, zahabu na vile vyombo, kisha tukavipatia kuhani Meremoti mwana wa Uria. Meremoti alikuwa pamoja na Eleazari mwana wa Finehasi, na Walawi wawili, Yozabadi mwana wa Yesua, na Noadia mwana wa Binui.
Walawi walikuwa: Yesua, Binui, Kadimieli, Serebia, Yuda na Matania, ambaye alishugulika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake.