Kwa hiyo, tufanye agano na Mungu wetu, tuachane na wanawake hawa pamoja na watoto wao, kwa kufuatana na shauri lako na la wengine wanaotii amri za Mungu. Yote yatendeke kwa kufuatana na Sheria.
Wayuda wanaoa wanawake wa kigeni na kuwaoea wana wao vilevile. Hivyo, taifa takatifu la Mungu limechanganyika na watu wa mataifa mengine. Vilevile wasimamizi na wakubwa ndio wa kwanza kutenda maovu hayo.”