Ezra 10:18 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200218 Hawa ndio makuhani waliooa wanawake wa kigeni: Wazao wa Yesua, wana wa Yehosadaki na wandugu zake: Maseya, Eliezeri, Yaribu na Gedalia. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Basi, watu wakaanza kazi katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili nyuma ya kufikia kwenye nyumba ya Mungu katika Yerusalema. Zerubabeli, mwana wa Saltieli, Yesua mwana wa Yosadaki, wandugu zao wengine, makuhani, Walawi na watu wengine wote waliorudi Yerusalema kutoka katika uhamisho, wakajiunga nao katika kazi hiyo. Walawi wote waliokuwa na umri wa miaka makumi mbili au zaidi, walichaguliwa kwa kusimamia kazi ya kuijenga upya nyumba ya Yawe.
Ezra, mwandishi, alikuwa akisimama kwenye mimbari ya mbao iliyotengenezwa kwa kusudi lile; na kwenye mukono wake wa kuume watu hawa walikuwa wakisimama: Matitia, Sema, Anaya, Uria, Hilkia na Masea; na kwenye mukono wake wa kushoto kulikuwa kunasimama watu hawa: Pedaya, Misaeli, Malkiya, Hasumu, Hasubadana, Zakaria na Mesulamu.