Wayuda walishinda waadui zao katika siku hizo, na katika mwezi huo huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha, na kilio chao kuwa sikukuu. Waliagizwa wakuwe wanazikumbuka siku hizo kwa kufanya karamu na sherehe, kupelekeana zawadi za chakula na kuwapa wamasikini vitu.
Hamani mwana wa Hamedata wa ukoo wa Agagi na adui wa Wayuda alikuwa amefanya mupango juu ya Wayuda kwa kuwaangamiza, vilevile alikuwa amepiga purimu, ni kusema kura, kwa kuamua siku ya kuwaponda na kuwaangamiza Wayuda.