Esteri 7:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20024 Maana, mimi na watu wangu tumeuzishwa kusudi tuuawe, tuangamizwe na kuteketezwa kabisa. Kama tungeuzishwa tu kuwa watumwa na wajakazi, ningekaa kimya wala nisingekusumbua. Ingawa tutateswa hakuna adui atakayeweza kulipa hasara hii kwa mufalme.” အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Wajumbe wakazipeleka barua hizo kwa kila jimbo katika utawala ule. Tangazo hilo lilisema kwamba kwa siku moja tu, ni kusema siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili unaoitwa Adari, Wayuda wote – tangia kwa vijana mpaka wazee, wanawake na watoto, wote wauawe, waangamizwe na kuteketezwa kabisa, na mali zao zote zinyanganywe.