Kisha, kiumbe kimoja chenye umbo la mutu, kiliigusa midomo yangu, nami nilifungua midomo yangu na kumwambia huyo aliyesimama karibu nami: Ee bwana, maono haya yameniletea maumivu makali hata nimeishiwa nguvu.
Lakini sasa, Danieli, weka kwa siri mambo hayo; funga kitabu na kutia muhuri juu yake mpaka wakati wa mwisho utakapofika. Wengi watakimbilia huko na huko, na maarifa yataongezeka.