Wafu wako wataishi tena, miili yao itafufuka. Wanaolala katika mavumbi wataamuka na kuimba kwa furaha! Mungu atapeleka umande wake wa uzima, nao wanaokuwa kwa wafu watatoka wazima.
Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowakula hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika hata kidogo. Watakuwa chukizo kwa watu wote.
Lakini wewe Yawe uko pamoja nami. Kwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha. Kwa hiyo watesaji wangu watajikwaa, nao hawataweza kunishinda. Watafezeheka kabisa, kwa sababu hawatashinda. Haya yao itadumu hata milele, nayo haitasahauliwa.
Kwa hiyo, toa unabii, uwaambie kwamba Bwana wenu Yawe anasema hivi: Enyi watu wangu, nitayafunua makaburi yenu na kuwafufua kutoka ndani ya makaburi yenu. Nitawarudisha ndani ya nyumba zenu katika inchi ya Israeli.
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!
Mufinyanzi anaweza kufanya sawa vile anavyotaka na udongo. Toka donge moja la udongo anaweza kutengeneza chombo kimoja cha heshima na kingine cha matumizi ya kawaida.
Nikaona wale waliokufa, wakubwa na wadogo wakisimama mbele ya kile kiti cha kifalme. Vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa ndicho kitabu cha uzima. Wale waliokufa wakahukumiwa kufuatana na matendo yao sawa vile ilivyoandikwa katika vitabu.