Amosi 8:12 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
12 Watu watatangatanga kutoka bahari hata bahari, kutoka upande wa kaskazini mpaka wa mashariki. Watakimbia huko na huko wakitafuta neno la Yawe, lakini hawatalipata.
Munapoendelea kutoa sadaka zenu na kuwateketeza watoto wenu kwa moto munajichafua mpaka leo hii. Nitaulizwa shauri nanyi, enyi watu wa Israeli? Kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe– sitakubali kuulizwa shauri nanyi.
Lakini sasa, Danieli, weka kwa siri mambo hayo; funga kitabu na kutia muhuri juu yake mpaka wakati wa mwisho utakapofika. Wengi watakimbilia huko na huko, na maarifa yataongezeka.
Wakati huo, kijana Samweli alipokuwa anamutumikia Yawe chini ya uangalizi wa Eli, ujumbe kutoka kwa Yawe ulikuwa mara haba tu; hata na maono kutoka kwake yalipatikana mara chache.