Amosi 6:12 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
12 Farasi wanaweza kukimbia katika mawe makubwa? Watu wanaweza kulima bahari na ngombe? Lakini ninyi mumeigeuza sheria kuwa sumu, na tunda la haki kuwa uchungu.
Ee Yawe, wewe unatafuta uaminifu siku zote. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa maonyo. Wamevifanya vichwa vyao kuwa vigumu kuliko jiwe; wamekataa kabisa kurudi kwako.
Lakini ninyi mumepanda uovu, ninyi mumevuna ubaya; mumekula matunda ya uongo wenu. Wewe Israeli ulitegemea nguvu zako mwenyewe, na wingi wa waaskari wako.
Wote ni wafundi wa kutenda maovu; waongozi na waamuzi wanaomba kituliro. Wakubwa wanaonyesha wazi nia zao mbaya, nao wanashirikiana pamoja kwa kuzitimiza.