Hata mukinitolea sadaka zenu za kuteketezwa kwa moto na za vyakula, mimi sitakubali kuzipokea; na sadaka zenu za amani za nyama wanono mimi sitaziangalia kabisa.
Nitazigeuza sikukuu zenu kuwa kilio, na nyimbo zenu za furaha kuwa maombolezo. Nitawavalisha ninyi wote magunia kwa huzuni na kunyoa vichwa vyenu upaa, kama kuomboleza kifo cha mutoto wa pekee. Na siku ya mwisho itakuwa ya uchungu mukubwa.