Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Amosi 5:22 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

22 Hata mukinitolea sadaka zenu za kuteketezwa kwa moto na za vyakula, mimi sitakubali kuzipokea; na sadaka zenu za amani za nyama wanono mimi sitaziangalia kabisa.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Amosi 5:22
19 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Nitakutolea sadaka za shukrani. Nitaomba kwa jina la Yawe.


Ee Yawe, Mungu wangu, umetufanyia maajabu mengi, na mipango yako juu yetu haihesabiki; hakuna yeyote anayekuwa kama wewe. Kama ningeweza kusimulia hayo yote, hesabu yake ingenishinda.


Anayenitolea shukrani kama sadaka yake, huyo ndiye anayenitukuza; yeyote anayedumu katika njia yangu, huyo ndiye nitakayemwokoa.”


Sadaka ya waovu ni chukizo kwa Yawe, lakini maombi ya watu wa usawa yanamufurahisha Mungu.


Sadaka ya mwovu ni kitu cha kuchukiza sana. Inachukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya.


Yawe anasema hivi: Uwingi wa sadaka zenu ni kitu gani kwangu? Nimechoka na sadaka zenu za kondoo wenye kuteketezwa na mafuta ya nyama wenu wenye kunona. Sipendezwi na damu ya ngombe dume, wala ya wana-kondoo, wala ya beberu.


Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: wananitolea sadaka ya ngombe na tena wanaua watu kwa kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwana-kondoo na vilevile wanaua imbwa. Wananitolea sadaka ya unga na vilevile wanatolea damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.


Yawe anasema hivi juu ya watu hawa: Kweli wamependa sana kutangatanga, wala hawakujizuia; kwa hiyo mimi Yawe sipendezwi nao. Sasa nitayakumbuka makosa yao, na kuwaazibu kwa ajili ya zambi zao.


Kwa nini kuniletea ubani kutoka Seba, na udi wa harufu nzuri kutoka inchi ya mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa kwa moto hazikubaliki, wala sadaka zenu zingine hazinipendezi.


Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Muongeze sadaka zenu za kuteketezwa kwa moto juu ya sadaka zenu zingine, nanyi mujikulie nyama zile!


Hii ndiyo sheria ya ibada kuelekea sadaka za amani ambazo mutu anaweza kumutolea Yawe.


Muondoe mbele yangu kelele za nyimbo zenu! Sitaki kusikiliza muziki wa vinubi vyenu!


Kwa hiyo sasa enyi makuhani, mumwombe Mungu kusudi atuhurumie. Yawe wa majeshi anasema hivi: Ikiwa munamutolea matoleo ya aina hiyo, kweli atawakubali?


Halafu Samweli akamwambia: “Unazani kwamba Yawe anapendelea zaidi sadaka za kuteketezwa kwa moto na matoleo mengine, kuliko kuitii sauti yake? Hapana. Kumutii yeye ni bora kuliko matoleo na kumusikiliza kuliko kumutolea mafuta ya beberu.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ