Moabu, ulitumainia matendo yako na hazina zako, lakini sasa wewe vilevile utatekwa; mungu wako Kemosi atapelekwa katika uhamisho pamoja na makuhani na watumishi wake.
Maana mimi ninajua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa zambi zenu; ninyi munawatesa watu wema, munapokea kituliro na kuzuia wakosefu wasipate haki katika tribinali.
Farasi wanaweza kukimbia katika mawe makubwa? Watu wanaweza kulima bahari na ngombe? Lakini ninyi mumeigeuza sheria kuwa sumu, na tunda la haki kuwa uchungu.
Ninamwona atakayekuja, ninamwona, lakini hayuko karibu. Nyota itatokea kwa wazao wa Yakobo, atatokea mufalme kati ya Waisraeli. Kwa fimbo yake atapiga viongozi wa Wamoabu, atawaangamiza wazao wote wa Seti.