Hiyo ni siku ya kuwaangamiza Wafilistini wote, kukomesha musaada uliobakia kutoka Tiro na Sidona. Maana Yawe anawaangamiza Wafilistini, watu waliobaki wa kisanga cha Kafutori.
Ataunyanganya utajiri wako pamoja na biashara yako. Atazibomoa kuta zako na kuziangusha nyumba zako nzuri; mawe, mbao na udongo ulivyotumia kwa kujenga nyumba hizo watavitupa katika bahari.
Kwa wingi wa mabaya yako na udanganyifu katika biashara yako ulipachafua pahali pako pa kuabudia; kwa hiyo niliwasha moto kwako, nao ukakuteketeza, nami nikakufanya kuwa majivu juu ya inchi, mbele ya wote waliokuangalia.