5 Ninazani kwamba wale mitume wanaohesabiwa kuwa wakubwa zaidi hawanipiti kitu kabisa.
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa sawa hivi ninavyokuwa, na neema yake niliyopewa haikukuwa ya bure, lakini nilitumika zaidi sana kuliko mitume wote wengine. Hakika si mimi, lakini ni neema ya Mungu inayokuwa pamoja nami.