Basi, Elia aliposikia sauti hiyo, alijifunika uso kwa koti lake, akatoka na kusimama kwenye mulango wa pango. Halafu, akasikia sauti: “Elia! Unafanya nini hapa?”
Elia akaondoka, akamukuta Elisha mwana wa Safati akilima. Pale, kulikuwa makundi kumi na mbili ya ngombe dume wawiliwawili wakilima, na ngombe wawili wa Elisha walikuwa wa nyuma kabisa. Basi, Elia akavua koti lake na kumutupia.
Yawe atakausha guba ya bahari ya Misri, kwa pumzi yake inayochoma atakausha muto Furati, nao utagawanyika katika vijito saba, watu wavuke humo miguu mikavu.
Kwa njia ya imani, Waisraeli walivuka bahari Nyekundu kama vile ingekuwa katika inchi kavu. Lakini wakati Wamisri walipojaribu kufanya vile, walizama na kufa ndani ya maji.
Wengine waliuawa kwa kutupiwa mawe, wengine walikatwa vipandevipande kwa misumeno, au kuuawa kwa upanga. Walitangatanga wakivaa ngozi za kondoo au za mbuzi, wakiishi katika umasikini, wakiteswa na kutendewa vibaya.
Malaika wa sita akamwanga kikombe chake katika muto mukubwa Furati. Maji yake yakakauka kusudi njia itengenezwe kwa ajili ya wafalme wanaotoka mashariki.