Elia akaondoka, akamukuta Elisha mwana wa Safati akilima. Pale, kulikuwa makundi kumi na mbili ya ngombe dume wawiliwawili wakilima, na ngombe wawili wa Elisha walikuwa wa nyuma kabisa. Basi, Elia akavua koti lake na kumutupia.
Elisha alipoona tukio hilo, akalia: “Baba yangu, baba yangu! Ulikuwa wa lazima kuliko magari ya Israeli na wapanda-farasi wake!” Basi, Elisha hakumwona tena Elia. Halafu Elisha akashika nguo zake na kuzipasua vipande viwili.
Wengine waliuawa kwa kutupiwa mawe, wengine walikatwa vipandevipande kwa misumeno, au kuuawa kwa upanga. Walitangatanga wakivaa ngozi za kondoo au za mbuzi, wakiishi katika umasikini, wakiteswa na kutendewa vibaya.